Jamii ya wenye ualbino wapaza sauti kuelekea chaguzi zijazo
1 October 2024, 7:52 pm
Na Nazael Mkude.
Kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji Nchini wito umetolewa kwa jamii kuacha tabia ya kuhusisha imani za kishirikiana katika mafanikio ya kisiasa.
Mwenyekiti wa Chama cha Watu wenye Ualbino Mkoa wa Dodoma Bwn. Lodovick Julius wakati akizungumza na Dodoma TV ofisini kwake mapema wiki hii, ameitaka jamii kuacha vitendo vya ubaguzi ikiwemo kuwaona watu wenye ualbino kuwa wanaweza kumsaidia mgombea kupata mafanikio ya kisiasa.
Kwa upande wake mjumbe wa chama cha watu wenye ualbino mkoa wa Dodoma Bi Magreth amesema elimu inapaswa kutolewa kwa jamii iliyo na mtazamo hasi kuhusu watu wenye ulbino ili kuondoa kasumba hiyo.
Dhana potofu kuhusu watu wenye ualbino kuwa wanaweza kutumika kishirikina kuwasaidia wagombea wa kisiasa kushinda chaguzi zijazo kunasababisha wasiwasi na hofu ya usalama wa jamii hiyo kutokana na kufanyiwa vitendo vya kikatili na baadhi ya watu miongoni mwa jamii.