Dodoma FM

Zuzu yaiomba JICA huduma ya maji zaidi

30 September 2024, 7:10 pm

Wananchi wa mtaa wa Mazengo Kata ya Zuzu wameliomba Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) kuwaongeza upatikanaji zaidi ya huduma ya maji kufuatia ukarabati wa kisima cha maji uliofanywa na shiirika hilo.

Na Mindi Joseph.

Licha cha ya Ukarabaiti huo ambao kwa sasa unawanufaisha wananchi takribani 4250 kuondokana na adha ya ya maji, wananchi hao wameomba kuongezwa upatikanaji zaidi wa ya huduma ya maji. Kisima hiki kwa sasa kinasambaza maji safi na Salama katika vituo 12 na wananchi 33 wameunganishwa moja kwa moja katika nyumba zao.

Sauti za wananchi

Mwenyekiti wa mtaa wa mazengo kata ya Zuzu Joshua Kajembe amesema kuwa kutokana na kuongezeka kwa watumiaji wa huduma ya maji hivyo wanaiomba JICA kuongeza upatikanaji zaidi wa huduma ya maji.

Mwenyekiti wa mtaa wa mazengo kata ya Zuzu Joshua Kajembe
Sauti ya Bwn. Joshua Kajembe

Kaimu Meneja wa RUWASA Wilaya ya Dodoma Mohamend Mbaga pamoja na fundi wa mradi huo wa maji Zuzu Emmanuel Mdosa walikuwa na haya ya kusema.

Kaimu Meneja wa RUWASA Wilaya ya Dodoma Mohamend Mbaga
Sauti ya Bwn. Mohamend Mbaga pamoja na Emmanuel Mdosa .

Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japani (JICA) linatekeleza miradi ambayo inafadhiliwa na Serikali ya Japani katika nchi zaidi ya 150 zinazoendelea.