Dodoma FM

Migahawa Hombolo yavutia kwa usafi

18 September 2024, 7:42 pm

Picjha kuonesha moja ya mgahawa , Hombolo

Wanafunzi kutoka Chuo cha Serikali za Mtaa Hombolo wanasema hali ya usafi kwa baadhi ya watoa huduma ya chakula imeimarika.

Na Mindi Joseph.

Suala la usafi jambo ni muhimu katika kujikinga dhidi magonjwa yasababishwayo na uchafu.  Hivyo ni jambo la msingi kila mmoja wetu kuhakikisha kuwa anazingatia tararibu za usafi ikiwemo kunawa mikono kwa maji safi tiririka na sabuni mara kwa mara hasa baada ya matumizi ya maliwato, kabla na baada ya kula hata pia kabla ya kuanza mapishi.

Katika kitongoji cha Hombolo jijini Dododma, ni  eneo ambalo limebahatika  kuwa na migahawa mingi ambapo wateja wake kwa  asilimia kubwa ni wanafunzi kutoka Chuo cha Serikali za Mtaa Hombolo wanasema hali ya usafi kwa baadhi ya watoa huduma ya chakula imeimarika.

Picha kuonesha moja ya wananchi akizungumzia suala la usafi kwa Mamalishe
Sauti za wananchi

Kwa upande wa wauzaji wa chakula Mama Lishe wanasema jukumu lao la kwanza ni kuhakikisha mazingira ya mgahawa yanakuwa safi  ili kuwalinda wananchi na magonjwa ya mlipuko..

Sauati za mama lishe , Haombolo
Picha kuonesha moja ya mteja akinawa mikono kwa maji tiririka na sabuni