Hombolo walalamikia changamoto ya barabara inayopelekea vyombo vya usafiri kuharibika.
21 April 2021, 8:29 am
Na ;Victor Chigwada
Wananchi wa Kata ya Hombolo Makulu Wilaya ya Dodoma mjini wametoa kilio chao juu ya changamoto ya barabara ambayo huwa inaathilika kwa kipindi cha mvua na kusababisha kero kwa watumiaji
Taswira ya habari imezungumza na Mwajuma Rashidi ambaye ni mkazi wa Hombolo na kusema kuwa wanaiomba Serikali iwasidie kuikarabati barabara hiyo ili kuepusha gharama za uharibifu wa vyombo vya usafili kutokana na matuta yaliyopo katika barabara hiyo
Mwenyekiti wa mtaa wa Hombolo A Bw. Geradi Mtagwa amekiri kukabiliwa na changamoto ya barabara na kuiomba serikali ifanye ukarabati kwa kiwango cha rami ili kupunguza kero ya marekebisho ya mara kwa mara
Mtagwa ameongeza kuwa kupitia kampeni za mwakajana za uchaguzi walipokea tamko kuwa tayari barabara hiyo imeingizwa kwenye mpango wa utekaelezaji
Naye mtendaji Kata wa Hombolo Makulu Bw.Wilisoni Nyenge amesema kuwa Hombolo ni moja ya maeneo yenye abiria wengi lakini adha ya barabara imekua ni tatizo na kuwashauri TARULA wanapofanya ukarabati waweke mifereji ya maji ili kusadia barabara hizo kuharibiwa na maji
Wakazi wa Hombolo wanategemea uchumi wao kwa shughuli za kilimo cha ,Mtama ,Ufuta,Zabibu pamoja na Uvuvi wa samaki katika bwawa la Hombolo na kusafirisha sehemu za mijin