Ardhi iliyo rasimishwa inasaidia kuleta maendeleo
7 August 2024, 6:19 pm
Wizara imeanzisha Kampeni maalumu kwa ajili ya kumsaidia Mwanamke katika umiliki wa Ardhi.
Na Fred Cheti.
Inaelezwa kuwa Ardhi iliyopangwa, kurasimishwa na kupimwa vizuri inasaidia kwa kiwango kikubwa kuleta maendeleo kwa Wananchi kutokana na kuruhusu shughuli za kiuchumi ndani ya Miji na Vijiji kuendelea bila kikwazo.
Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Lucy Kabyemela wakati akifanya mahojiano maalumu na Dodoma TV kuhusu umuhimu wa Jamii kurasimisha Makazi holela kwa Maendeleo ya kiuchumi katika Banda la Wizara hiyo kwenye maonesho ya Nanenane yanayoendelea Jijini hapa.
Katika hatua nyingine Naibu Katibu Mkuu huyo amesema Wizara imeanzisha Kampeni maalumu kwa ajili ya kumsaidia Mwanamke katika umiliki wa Ardhi inapotokea mwenza wake amefariki ili kuondoa changamoto iliyopo.
Nae Mmoja wa Wananchi aliyefika kupata Elimu kuhusu urasimishaji Ardhi alikua na haya ya kusema.