Dodoma FM

Barabara ya Pembamoto na Mlali kupandishwa hadhi

23 July 2024, 3:30 pm

Picha ni moja barabara iliyopo wilayani Kongwa ambayo ipo katika kiwango cha lami.Picha na Bernadetha Mwakilabi.

Ameahidi kuunganisha wilaya ya jirani ya Gairo kupanda hadhi kutoka kwa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini Tanzania (TARURA) kwenda kwa wakala wa barabara Tanzania (TANROADS) ili kuunganisha mikoa.

Na Bernadetha Mwakilabi, Kongwa
Mbunge wa Jimbo la Kongwa Mh. Joab Ndugai ameahidi kuwa ataendelea kufuatilia ahadi iliyotolewa ya kuipandisha hadhi barabara ya kutoka Kijiji Cha Mlali kwenda kijiji Cha Pembamoto.

Mh. Ndugai ameeleza hayo alipokuwa katika kijiji Cha Pembamoto katika ziara yake ya kutembelea miradi ya maendeleo kwenye vijiji na kata wilayani humo ili kuona utekelezwaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) ambapo amesema kuwa barabara hiyo inaunganisha mikoa miwili ya Dodoma na Morogoro.

Sauti ya Mh. Joab Ndugai .

Akitoa ufafanuzi wa barabara hiyo Mhandisi Boniface Mandi kutoka wakala wa barabara za vijijini na mijini (TARURA) wilaya Kongwa amesema kuwa tayari shilingi milioni 120 zimeshatengwa katika bajeti ya mwaka 2024/2025 kwa ajili ya matengenezo ya Barabara ya Pembamoto-Chiwe na kipande cha Pembamoto kwenda Lubeho mkoani Morogoro kitafanyiwa kazi, hii ni baada ya kuharibiwa vibaya na mvua za elnino.

Mhandisi Boniface Mandi ameongeza kuwa TARURA inahitaji ushirikiano baina yao na wananchi ili kuafikiana juu ya njia sahihi ya kuchepusha maji kupita katika mashamba yao ili barabara isiweze kuharibika tena pindi itakapotengenezwa.

Sauti ya Mhandisi Boniface Mandi .

Aidha ameweka wazi kuwa kazi ya kumtafuta mkandarasi wa kutengeneza barabara hiyo ipo kwenye hatua za mwisho ambapo hadi kufikia mwezi disemba mwaka huu kazi itakuwa imeanza mara moja.
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Kongwa Mh White Zuberi ameeleza kuwa mara tu halmashauri ya wilaya Kongwa itakapopata kibali cha kuongeza Kata itakipa hadhi Kijiji Cha Pembamoto na kuwa Kata ili kuchochea zaidi maendeleo kwa wananchi.

Pamoja na changamoto za afya, maji, umeme, na miundombinu kuendelea kufanyiwa kazi lakini Mhandisi Boniface Mandi amekemea vikali changamoto ya elimu ambapo wazazi huwazuia watoto wao kufaulu mitihani yao ya Taifa ili wakafanye kazi za ndani jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo ya mkoa na ni ukiukwaji wa haki za watoto.

Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Kongwa Mh White Zuberi ameeleza kuwa mara tu halmashauri ya wilaya Kongwa itakapopata kibali cha kuongeza Kata itakipa hadhi Kijiji Cha Pembamoto na kuwa Kata ili kuchochea zaidi maendeleo kwa wananchi.

Pamoja na changamoto za afya, maji, umeme, na miundombinu kuendelea kufanyiwa kazi lakini Mh Zuberi amekemea vikali changamoto ya elimu ambapo wazazi huwazuia watoto wao kufaulu mitihani yao ya Taifa ili wakafanye kazi za ndani jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo ya mkoa na ni ukiukwaji wa haki za watoto.

Sauti ya Mh. White Zuberi.