Wafanyabiashara watakiwa kusajili majina na alama za biashara zao
21 June 2024, 5:58 pm
Sheria inamuhitaji kila mfanya biashara ajirasimishe kwasababu ukirasimisha biashara yako unapata faida nyingi ikiwa pamoja na kupata tenda mbali mbali za serikali na sekta binafsi.
Mindi Joseph.
wajasiriamali na wafanyabiashara nchini wametakiwa kusajili na kurasimisha majina na alama za biashara ili kujiendesha kihalali na kutambulika katika masoko katika kukuza uchumi.
Mifumo ya TEHAMA inawezesha kusajili huduma zao ili wafanye biashara zao kwa kufuata taratibu na sheria zilizowekwa na nchi kama anavyozungumza Kaimu Meneja Rasilimali watu na utawala Migisha Kahangwa kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni.
Kwa upande wake afisa usajili kutoka wakala wa usajili leseni BRELA Gabriel Girangay amesema kuwa wamekuwa wakitembelea wafanyabiashara katika maeneo yao ili kutatua changamoto mbali mbali ikiwemo ya elimu juu ya mifumo yao.
Usajili wa biashara ni ulinzi wa kisheria ambao unawasaidia wafanyabiashara kuondokana na changamoto za kibiashara zinazoweza kujitokeza kama wanavyosema.