Serikali kuendelea kutambua mila na tamaduni za Kitanzania
18 June 2024, 5:35 pm
Sherehe za utamaduni wa kabila la wagogo maarufu kama Tambiko hufanyika kila mwaka kwa lengo la kuomba Baraka kwa Mwenyezi Mungu.
Na Anselima Komba.
Serikali imesema inatambua mila na tamaduni za kitanzania na itaendelea kuzienzi kwa kutambua mchango mkubwa unaotolewa kwa serikali kupitia viongozi wa mila hizo katika maeneo mbalimbali Nchini.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Alhaji Jabir Shekimweri amesema hayo katika viwanja vya makumbusho ya Mkoa wa Dodoma himaya ya bwibwi kata ya Iyumbu wakati wa sherehe za utamaduni wa kabila la wagogo maarufu kama Tambiko ambalo linafanyika kila mwaka kwa lengo la kuomba Baraka kwa Mwenyezi Mungu na kuita mvua kwa msimu ujao.
Kwa upande wake Chifu Fadhili kutoka Mkoa wa Kigoma ameishukuru serikali ya awamu ya 6 chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuheshimu mila na desturi za kitanzania.
Afisa sheria Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya Meshack Lyabonga amewaomba machifu wote nchini kuendeleza mapambano dhidi ya madawa ya kulevya ili kuokoa kizazi cha sasa na baadae.
Afisa ustawi wa jamii mwandamizi kutoka wizara ya maendeleo ya jamii Averino Chaula amevipongeza vikundi vya utamaduni kwa kuitambua wizara ya maendeleo ya jamii kama wadau muhimu wa kuendeleza mila za Tanzania.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri amsema hayo katika viwanja vya makumbusho ya Mkoa wa Dodoma himaya ya bwibwi kata ya Iyumbu wakati wa