Wizara ya Elimu kutumia matokeo ya utafiti wa HakiElimu
4 June 2024, 5:34 pm
Utafiti huu utasadia katika kufanya maamuzi kuhusu upatikanaji wa elimu mijini katika eneo la Afika Mashariki.
Na Mindi Joseph.
Wizara ya Elimu imesema itahakikisha inatumia matokeo ya utafiti wa HakiElimu katika kuhakikisha kuwa upatikanaji wa elimu unakuwa sawa kwa makundi yote.
Uzinduzi wa utafiti huu unaohusu upatikanaji wa elimu bora kwa watoto wanaoishi kwenye makazi duni mijini umekuja wakati muafaka hasa kwa kuzingatia ukuaji wa kasi wa miji unaotokana na ongezeko kubwa la watu wanaohama kutoka vijijini kwenda mijini.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mkurugenzi Udhibiti Ubora Wizara ya Elimu Ephraim Simbeye Wizara ya Elimu amesema wanatambua umuhimu wa tafiti na hivyo wameanzisha utaratibu ambao watafiti wataweza kuwasilisha taarifa za tafiti katika Wizara ya Elimu.
kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu, Dkt John Kalage amesema wamefanya utafiti huu kwa lengo la kupata hali halisi ya upatikanaji wa elimu katika maeneo ya mijini.