Nayu watakiwa kuwa tayari zoezi la urasimishaji ardhi
28 May 2024, 5:45 pm
Kila mwananchi ambaye anamiliki ardhi atafikiwa na zoezi hilo hivyo ni muhimu kila mmoja kushiriki.
Na Victor Chigwada.
Wakazi wa kijiji cha Nayu wilayani Chamwino mkoani Dodoma wametakiwa kuwa tayari kwa ajili ya zoezi la urasimishaji ardhi na makazi ambalo linatarajia kuanza hivi karibuni.
Wito huo umetolewa na Afisa Mtendaji wa kijiji hicho Nyarusanda Julius wakati akielezea fursa ya mradi huo kwa wananchi ambapo amesema ni vyema kila mwananchi kuwa tayari kwa ajili ya zoezi hilo
Aidha amesisitiza wawekezaji wa ardhi katika kijiji hicho nao kuhakikisha wanashiriiki zoezi hilo ili kupata hati miliki .
Kwa upande mwingine amesema kuwa tayari hatua za awali za mradi zimeanza kutekelezwa ikiwa ni pamoja na uwekaji wa mabango katika maeneo ya huduma za kijamii.
Yapi mapokeo ya wananchi kuhusu mradi huo,hawa ni baadhi ya wananchi wa kijiji cha Nayu wakizungumza tija ya mradi huo katika kupandisha thamani ya Ardhi zao