Uzalishaji wa maji Nzuguni waongeza asilimia 11.7 ya maji
27 March 2024, 5:10 pm
Mradi wa Maji Nzuguni umegharimu bilion 4.3 lengo likiwa ni kuboresha huduma ya usambazaji maji katika kata na jiji la Dodoma kwa ujumla.
Na Mindi Joseph.
Kukamilika kwa Mradi wa awamu ya kwanza wa Visima 5 vya maji Eneo la nzuguni umeongeza asilimia 11 .7 ya maji yanazalishwa kutoka lita 68,600,000 hadi 76,000,000 kwasiku.
Visima 5 vya mradi huo vinahudumia wananchi elfu 75000 huku visima vitano vya awamu ya pili vikitarajia kuhudumia maeneo ya kisasa,nyumba 300 na maeneo mengine.
Mhandisi wa maji Duwasa James Rioba anasema mradi huu wa maji ndio mkubwa kwa mwaka huu wa fedha.
Miongoni mwa wananchi wamepongeza mradi huo kwa kuwatatulia changamoto ya maji.
Mwenyekiti wa mtaa wa Nzunguni A Onaely Mbatiani anasema Mradi wa maji nzuguni umemaliza changamoto ya maji kwa wananchi wake.