Wajawazito Handali walazimika kwenda leba na maji
15 February 2024, 4:27 pm
Pamoja na hatua hizo za kwenda na maji kituo cha afya lakini bado wanakutana na shuruba nyingine namna ya kupata maji hayo bombani.
Na Victor Chigwada.
Pamoja na umuhimu wa matumizi ya maji katika sehemu za kutolea huduma za afya imekuwa tofauti kwa kituo cha Handali ambapo kwa kiasi kikubwa upatikanaji maji umekuwa changamoto kubwa kituoni hapo.
Hayo yameelezwa na baadhi ya wakazi wa Handali nakusema kuwa licha ya changamoto ya maji mtaani hali hiyo imekuwa ikiwaathiri hata waendapo kituo cha afya kupata huduma.
Wamesema zipo nyakati ambazo huwalizimu wazazi wanaoshikwa na uchungu wa kujifungua kwenda kituoni na maji yao binafsi.
Naye Mganga mfawidhi wa kituo cha Handali Dk.Enock Katalasita amekiri kuwepo kwa changamoto ya maji kituoni hapo na kuwalazimu kutumia maji ya mtu binafsi.