Watoto wadaiwa kutumika biashara ya dawa za kulevya
31 January 2024, 10:08 pm
Watoto wamekuwa wakitumiwa kusafirisha dawa hizo na kuwasababishia athari mbalimbali.
Na Thadei Tesha.
Kundi la watoto limetajwa kutumika kwa sehemu kubwa katika biashara haramu ya usafirishaji wa dawa za kulevya nchini.
Hayo yamesemwa na kamishna Jenerali wa Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya nchini Aretas Lyimo wakati akizungumza katika maadhimisho ya wiki ya sheria katika viwanja vya nyerere square Jijini Dodoma..
Amesema kuwa watoto wamekuwa wakitumiwa kusafirisha dawa hizo na kuwasababishia athari mbalimbali watoto hao huku wazazi wakisisitizwa kuzingatia wajibu wa kuhakikisha wanawalinda watoto wao dhidi ya biashara hiyo.
Veridiana Mlimba ni Mkaguzi Msaidizi wa polisi kutoka makao makuu ya jeshi la polisi anaeleza mikakati ya jeshi la polisi ya kuwabaini wahusika wakuu wa biashara hiyo na kuhakikisha watoto wanaondolewa katika utumikishwaji wa biashara hiyo.
Lakini ni upi mtazamo wa wazazi Jijini hapa katika kukabiliana na changamoto hii?