Serikali kukamilisha miradi ya kilimo iliyo anzisha
14 April 2021, 1:09 pm
Na; Selemani Kodima
Wizara ya kilimo imesema itaendelea kujikita zaidi kwenye kipaumbele cha kufanya tathimini na kukamilisha miradi ya umwagiliaji iliyopo ikiwemo kuangalia ufanisi wake na kukamilishi miradi ya maji ambayo wameshaianza.
Hayo yamesemwa leo bungeni na Naibu waziri wa kilimo Hussen Bashe wakati akijibu swali la Nyongeza la mbunge wa jimbo la Muleba kusini Oscar Kikoyo, ambapo amesema kuwa serikali kupitia wizara ya kilimo hawategemei kuja na mradi mpya wa umwagiliaji isipokuwa kukamilisha miradi waliyoianza.
Naibu waziri Bashe amesema moja ya kipaumbele cha serikali ni kuwekeza katika uzalishaji wa mbegu ambapo serikali ina mashamba 13 ambayo yatapewa kipaumbele katika bajeti ya mwaka ujao ili kuwezesha kuzalisha mbegu bora.
Aidha Akitoa ufafanuzi juu swali la nyongeza la Mbunge Mwantum Zodo ,Naibu Waziri mesema Wizara inaendela kubadilisha mwogozo wa tume ya umwagiliaji huku pia kupitia kuwekeza katika ununuzi wa vifaa ambavyo tume hiyo itaweza kutumia kuchimba mabwawa na kujenga miradi ya umwagiliaji kwa mfumo wa mapato ya ndani (force account)