Wananchi Chamwino waiomba serikali kudhibiti tembo wanaovamia makazi yao
20 November 2023, 7:15 pm
Wananchi hao wanasema uvamizi wa wanyama hao unahatarisha maisha yao pamoja na mali zao.
Na Seleman kodima.
Wananchi wa kata za Manda, Fufu na Mlowa Bwawani wilayani Chamwino mkoani Dodoma wameiomba serikali kudhibiti tembo ambao wamekuwa wakivamia makazi ya watu na kufanya uharibifu wa nyumba za makazi pamoja na mazao mashambani hali ambayo inahatarisha usalama wao
Ombi hilo limetolewa na madiwani wa kata hizo kwa niaba ya wananchi katika kikao cha baraza la madiwani la halmashauri ya chamwino ambapo wameomba serikali kutafuta suluhu ya kudumu ya kudhibiti wanyama hao
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya chamwino bwana edson gerald amesema watashirikiana na mamlaka zinazohusika na wanyamapori ili kulinda usalama wa wananchi wa maeneo hayo…
Akizungumza na Taswira ya Habari kwa njia ya simu juu ya kadhia hiyo afisa habari wa Mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania tawa Bwana Beatus Maganja ameeleza mikakati ya mamlaka hiyo…