Wakazi wa Karume waomba kuwekewa alama za vivuko barabarani
5 September 2023, 4:01 pm
Wananchi wanadai kukosekana kwa alama za barabarani katika eneo hilo kunapelekea baadhi ya watu kuendesha vyombo vya moto kwa kasi na kupelekea ajali za mara kwa mara.
Na Asted Bambora.
Imeelezwa kuwa ukosefu wa AIama za Barabarani hususani mchoro wa Pundamilia katika Eneo la Kwamudi, Mtaa wa Karume jijini Dodoma ni sababu ya uwepo wa ajali za mara kwa mara katika eneo hilo .
Wakizungumza na Kituo hiki baadhi ya wananchi wa mtaa wa karume uliopo kata ya Mailimbili jijini Dodoma wameiomba Serikali kupitia uongozi wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROAD) kuweka Alama za Barabarani ikiwemo michoro ya Pundamilia,Alama za Matuta katika Barabara itokayo Dodoma kuelekea Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro ili kupunguza ajali .
Bwn.Hussein Shosho ni Dereva Bodaboda katika mtaa huo ameomba mamlaka inayohusika kuweka Alama za Barabarani kuwasaidia kuweka alama hizo katika eneo la kwa Mudi ili kupunguza mwendo kasi wa vyombo vya moto.
Kwa upande wake , Mwenyekiti wa Mtaa wa Karume Bw.Matwiga Kyatya amekiri kuwepo kwa ajali nyingi katika eneo hilo huku akitaja chanzo kuwa ni ukosefu wa Alama za Barabarani .