Dodoma FM

Wasimamizi wa ujenzi shule ya sekondari Msalato watakiwa kuongeza kasi

18 July 2023, 2:39 pm

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma mh Rosemary Senyamule akizungumza katika ziara yake ya kukagua ujenzi wa majengo ya sekondari Msalato hapo jana. Picha na Fred Cheti.

Mh. Senyamule ameonesha kuridhishwa na utekelezaji wa ujenzi huo ambapo ametoa rai kwa wasimamizi kuongeza kasi ili yakamilike kabla ya tarehe 30 Mwezi huu.

Na Fred Cheti.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ameridhishwa na utekelezaji wa ujenzi wa madarasa 7 katika shule ya Sekondari ya wasichana ya Msalato huku akiwataka wasimamizi kuongeza kasi zaidi.

Mhe. Senyamule ameyasema hayo leo katika ziara yake shuleni hapo ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa madarasa hayo unaofadhiliwa kupitia mradi wa (BOOST) ambapo ameoneshwa kuridhishwa na utekelezaji wake huku akitoa rai kwa wasimamizi kuongeza kasi ili yakamilike kabla ya tarehe 30 Mwezi huu.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri amesema ongezeko la madarasa hayo itakua ni chachu kwa shule hiyo kufanya vizuri zaidi kwani ni moja ya shule zinazoubeba mkoa wa Dodoma kwa kufanya vizuri.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Dodoma.
Picha ni wanafunzi wa shule ya Sekondari ya wasichana Msalato jijini Dodoma. Picha na Fred Cheti.

Nao baadhi ya wanafunzi katika shule hiyo wameishukuru serikali kwa mradi wa ujenzi wa madarasa hayo wani itawapunguzia adha ya uhaba wa madarasa huku wakiahidi kufanya vizuri katika mitihani hayo.

Sauti za wanafunzi wa shule ya sekondari Msalato.

CLIP 3….WANAFUNZI SHULE MSALATO