Wananchi watakiwa kutumia mabwawa yanayojengwa kujikita katika kilimo cha umwagiliaji
19 May 2023, 7:36 pm
Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma imefanyika wilayani Bahi lengo likiwa ni kutembelea miradi mbalimbali wilayani humo ikiwemo ujenzi wa shule ya msingi Ngondo, nyumba ya mwalimu na mradi wa umwagiliaji Kongogo.
Na Mariam Kasawa.
Wananchi wametakiwa kutumia vizuri mabwawa yanayo jengwa kwaajili ya kilimo cha umwagiliaji ili waweze kuachana na kilimo cha kubahatisha.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa mkoa wa Dodoma Bi. Rosemary Senyamule alipo kuwa akizungumza na wakazi wa kata ya Babayu kijiji cha Kongogo wilayani Bahi alipofanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo wilayani humo.
Bi Senyamule amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha wananchi wanaachana na kilimo cha kubahatisha na kujikita katika kilimo cha umwagiliaji .
Mkuu wa Mkoa alitoa nafasi kwa wananchi wa kata hiyo kutoa kero zao mbalimbali ambazo zilipatiwa majibu na wataalamu.
Kwa upande wake Mkuu wa wialaya ya Bahi Mh. Godwin Gondwe akisoma taarifa ya kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma amesema wamejiwekea mkakati wa kukamilisha miradi mapema .