TMO yawasilisha rasimu ya ujenzi wa kituo cha michezo Mbande
17 May 2023, 4:51 pm
Kwa mujibu wa viongozi wa Taasisi hiyo ujenzi wa Kituo hicho utaleta tija kwa wananchi kwani utahusisha maeneo ya vitega uchumi mbalimbali yakiwemo maduka na huduma nyinginezo.
Na Alfred Bulahya.
Taasisi ya Tembea Kwa Matumaini Organization (TMO) imewasilisha rasimu ya ujenzi wa Kituo cha michezo kinachotarajiwa kujengwa katika Kijiji cha Mbande Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma.
Kwa mujibu wa rasimu ya awali iliyowasilishwa na msanifu Fadhili Ally Namkumbe kutoka Place plan Consultant, ujenzi utagharimu takribani shilingi bil 12.
Mkurugenzi Mtendaji Halmahauri ya Wilaya ya Kongwa Dkt. Omary A. Nkullo kwa kushiirikiana na wakuu wa Divisheni na vitengo sanjali na wajumbe wa kamati ya ulinzi na Usalama, wameridhia mpango huo.
Mkurugenzi wa Taasisi hiyo (TMO) Bwana Mohamed Hemed, ametoa shukrani za pekee kwa wajumbe wa kikao hicho cha kupitisha rasimu na ameahidi shughuli za ujenzi kuanza mara moja.