Serikali yazindua kampeni ya kulinda maadili
16 May 2023, 10:56 am
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma amepongeza juhudi za Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wanawake na Makundi Maalum kwa juhudi za kutoa za Elimuu juu ya umuhimu wa Familia na Upendo katika Jamii zetu.
Na Mariam Matundu.
Katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Familia, Mei 15, 2023, Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum imezindua Kampeni ya Kitaifa kuhakikisha maadili yanalindwa na kuendana na mila na desturi za nchi.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akizindua kampeni hiyo katika kongamano maalum, amesema jamii yenyewe inatakiwa kuwajibika kwenye malezi yanayoendana na miiko na tamaduni za kitanzania ili kuimarisha familia na kuepuka mmomonyoko wa maadili.
Mhe. Dkt. Gwajima amebainisha kwamba takwimu za vitendo vya ukatili hasa kwa watoto zinaonesha asilimia 60 ukatili unafanyika nyumbani hivyo msingi wa kwanza katika kutelekeza kampeni hiyo ni kuanzia ndani ya familia.
Awali mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ustawi na maendeleo ya jamii Fatma Toufiq amesema ili kuwa na bora na yenye ustawi ni muhimu familia ziwe na upendo na maadili pamoja na kumshirikisha Mungu.
Nae mwakilishi wa IGP Mrakibu Msaidizi wa Polisi Dkt Ezekiel Kyogo amesema ni muhimu familia ziwekeze katika malezi ili kulinda maadili hali itakayo saidia vyombo vya ulinzi na usalama kupunguza mzigo wa kupambana na wahalifu kwa kuwa taifa litakuwa na watu wenye maadili na uadilifu.
Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma amepongeza juhudi za Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wanawake na Makundi Maalum kwa juhudi za kutoa za Elimuu juu ya umuhimu wa Familia na Upendo katika Jamii zetu.
kauli mbiu katika maadhimisho hayo ni” LINDA MAADILI NA UPENDO KWA FAMILIA IMARA”.