Hospitali ya Benjamini Mkapa yazindua huduma ya upandikizaji Uloto
10 May 2023, 8:01 pm
Nchi ya Tanzania inashika nafasi ya 4 kuwa na wangojwa wengi ulimwenguni wa Selimundu huku wenye watoto Elfu 11000 kwa mwaka wanaweza kufa kabla ya kufikisha umri wa miaka 5 sawa na asilimia 50 hadi 90.
Na Mariam Kasawa.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali iliamua kuwekeza shilingi bilioni 2.7 ili kuanzisha huduma ya upandikizaji uloto na kupunguza gharama za matibabu hayo kwa wananchi.
Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo Leo katika Uzinduzi wa Huduma za upandikizaji uloto katika Hospital ya Benjamin Mkapa na ameitaka Wizara ya afya kuendela kuhakikisha Watoto wachanga wanaozaliwa wanapimwa ugonjwa wa selimudu.
Kwa upande wake Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amewataka Wazazi wenye watoto wenye ugonjwa wa selimundu kwenda kwa wataalamu.
Tayari huduma ya upandikizaji uloto imefanyika kwa watoto 3 wenye ugonjwa selimundu na hapa Watoto na wazazi Wanatoa ushuhuda.
Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali ya Benjamin Mkapa, Dkt. Alphonce Chandika anasema upandikizaji wa Uloto umefanyika kwa mara ya kwanza Tanzania na kuifanya Tanzania kuwa miongoni mwa Nchi 7 zinazotoa huduma hii.