Wawekezaji watakiwa kufanya tahmini ya athari za mazingira
5 May 2023, 2:45 pm
Na Fred Cheti.
Baraza la Usimamizi na uhifadhi wa Mazingira (NEMC) limewataka wawekezaji wote wa miradi ya maendeleo nchini kufanya tathimini ya athari kwa mazingira katika miradi yao ili kuepusha migogoro itakayotokana na uchafuzi wa mazingira.
Hayo yameelezwa na Bwn. Abel Sembeka Meneja wa tathmini ya athari za Mazingira katika baraza hilo ofisini kwake ikiwa ni sehemu ya kutoa elimu kwa wawekezaji wa miradi mbalimbali juu ya umuhimu wa kufanya tathmini hiyo ya athari kwa mazingira (TAM)
Bwana Sembeka amesema serikali kupitia baraza hilo itaendelea kutoa elimu kwa wawekezaji wote kuhusu suala la utunzaji wa mazingira ili ukuaji wa uchumi nchini unaochangiwa na wawekezaji uende sambamba na utunzaji wa mazingira.