Bodi ya nafaka yaendelea kuimarisha soko la mazao Dodoma
4 April 2023, 5:35 pm
Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko imefanikiwa kununua mazao ya wakulima yenye thamani ya Shilingi 9.6 Bilioni na kuzalisha Tani 480 zilizotolewa msaada Nchini Malawi.
Na Mindi Joseph.
Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko Mkoani Dodoma inaendelea kuimarisha Soko la wakulima hususani katika zao la Mahindi, Mtama, Alizeti pamoja na Mafuta ghafi.
Hayo yamebainishwa jijini Dodoma na Meneja wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko Lelansi Mwakibibi ambae amesema wanalenga kutengeneza soko la wakulima ili kuhakikisha hakuna urasimu wowote katika kununua mazao.
Kwa upande wake, Afisa masoko Mkuu wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko Tumpe manongi amesema Bodi imekuwa ikishirikiana na wakulima katika kuyaongezea thamani mazao.