Vijana wazungumzia changamoto za mikopo halmashauri
30 March 2023, 6:14 pm
Vijana hao wamesema kuwa kumekuwa na changamoto na usumbufu mkubwa kwani wanatumia muda mwingi kufuatilia fedha hizo.
Na Victor Chigwada .
Baadhi ya vijana wa kutoka Wilaya ya Chamwino wamezungumzia changamoto wanazozipata katika Halmashauri pindi wanapoenda kuchukua mikopo inayotengwa na serikali kwaajili yao
Aidha wameiomba Serikali kuongeza fungu la fedha katika Halimashauri nchini ili wapate fedha hizo sawa na mahitaji yao .
Joseph Mpilimi ni mwenyekiti wa kijiji cha Mlebe amekiri kuwa kumekuwa na changamoto katika kupata mikopo inayotengwa na serikali kupitia Halmashauri hali inayokatisha tamaa vijana
Naye Afisa maendeleo ya jamii wa Kata ya Msamaro Bi.Ng’washi Mhuli amesema kuwa bajeti za Halmashauri zimekuwa zikichangia vikundi kushindwa kutimiza malengo yao
Mhuli ameomba mashirika mbalimbali kuwasaiidia vijana kimawazo na hata kuwawezesha kifedha ili kuwanufaisha katika shughuli za vikundi vyao
Serikali imeweka mazingira wezeshi kwa vijana ,wanawake na watu wenye ulemavu ili waweze kujiajili na kushiriki katika shughuli za kimaendeleo kwa kutoa mikopo isiyo na riba.