Wanawake watakiwa kuacha kuwaficha watoto wenye ulemavu
6 March 2023, 12:29 pm
Baadhi ya vitu ambavyo vimekabidhiwa kwa watoto hao ni pamoja na magodoro,taulo za kike,mavazi,sabuni ,mafuta ya kupaka na vitu vingine ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa kila mwaka wa kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Na Seleman Kodima.
Wito umetolewa kwa wanawake mkoa Dodoma kuacha kuwaficha watoto wenye ulemavu ndani kwani kufanya hivyo ni kuwanyima haki zao za msingi .
Hayo yamesemwa na Katibu wa umoja wa wanawake mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira dodoma DUWASA Esther Mlewa wakati walipoitembelea shule ya msingi ya kingwe viziwi kwa ajili ya kutoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani
Kwa upande wake Afisa Elimu maalum wilaya ya Bahi Sarah Chizingwa amewakumbusha wanawake kuonesha upendo kwa watoto wenye ulemavu na kusisitiza upo umuhimu wa kuwapeleka watoto hao kupata elimu.
Nae mwalimu mkuu wa shule ya kingwe Viziwi Thadei Mwagila amesema kitendo cha wanawake hao kuwakumbuka watoto hao kinaleta faraja hali ambayo inawapa uthamani zaidi na kujiona nao ni sehemu ya jamii.
Diwani wa kata ya Kingwe Adon Mabalwe amewataka wanawake hao kuendelea kutoa elimu kwa wanawake wengine kujua umuhimu wa kusaidia makundi ya wahitaji pamoja na watoto wa kike