Dodoma FM

Mbugani watakiwa kukamilisha ujenzi wa madarasa kwa wakati

6 March 2023, 10:22 am

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Rosemary Senyamule akizungumza na uongozi wa shule ya msingi Mbugani. Picha na Mariam Kasawa.

Shule hiyo ambayo ni shule shikizi inatakiwa kukamilisha kwa wakati ujenzi wa madarasa mawili ambayo baada ya kukamilika kwake kutakuwa na jumla ya vyumba sita vya madarasa katika shule hiyo ya msingi Mbugani.

Na Fred Cheti.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh Rosemary Senyamule amewataka wasimamizi na uongozi wa shule ya Msingi Mbugani  iliyopo katika  kijiji cha Ngambi wilayani Mpwapwa kukamilisha kwa wakati   ujenzi wa  madarasa mawili katika shule hiyo ili kuepuka usumbufu..

Mh. Rosemary ameyasema hayo alipotembelea katika shule hiyo inayomilikiwa na kijiji hicho ambapo serikali imekipatia fedha ya kwa ajili ya kuongeza vyumba vya madarasa shuleni hapo akiwa  katika ziara yake wilayani Mpwapwa kukagua maendeleo ya miradi mbalimbali inayotekelezwa wilayani humo.

Sauti ya Mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule.

Aidha Mh Rosemary  ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa wazazi wilayani humo kua na mwamko wa kuwaandikisha watoto ili kufikia asilimia mia moja badala ya silimia 80 iliyopo mpka sasa wilayani humo.

Sauti ya Mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule