Dodoma FM
Wanawake watakiwa kuacha kukimbilia mikopo Mitaani
24 February 2023, 3:47 pm
Mikopo mingi ya mitaani imekuwa inapelekea kukosa faida na kushindwa kujiwekea akiba
Na Mariam Kasawa.
Wanawake wametakiwa kuacha kukimbilia mikopo ya Mitaani badala yake wajikite kuomba mikopo inayo tolewa na halmashauri ili waweze kunufaika na mikopo hiyo.
Akizungumza na Dodoma Tv Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Jiji la Dodoma Bi. Charity Sichona amesema marejesho ya mikopo mingi ya mitaani imekuwa inapelekea kukosa faida na kushindwa kujiwekea akiba kutokana na marejesho.