Wananchi waomba elimu Umiliki ardhi
18 January 2023, 2:03 pm
Na; Mariam Matundu.
Wananchi jijini Dodoma wamesema kuwa elimu ya umiliki wa ardhi inatakiwa kutolewa kwa jamii ili kupunguza migogoro ya ardhi inayojitokeza maeneo mbalimbali.
wakizungumza na Taswira ya habari wamesema baadhi ya wananchi hawajui ni kwanamna gani wanaweza kuwa salama na milki zao za ardhi na ndio sababu ya kutokea kwa migogoro hiyo.
hapo jana Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kushirikiana na benki ya Dunia imezindua Mradi wa Uboreshaji wa Usalama wa Milki za ardhi huku dhamira kuu ya mradi huo ikiwa ni kuboresha usalama wa milki za ardhi na utoaji huduma kwa wananchi.
Naibu waziri wa Ardhi Mh. Ridhiwani Kikwete ameeleza manufaa ya mradi huo kuwa ni pamoja na kuboresha usalama wa milki za ardhi .
Miongoni mwa Mikoa ambayo itanufaika na mradi huu katika utoaji wa hatimiliki pamoja na leseni za makazi ni Dodoma .