Dodoma FM

Wadau watakiwa kupaza sauti dhidi ya vitendo vya ukatili

19 December 2022, 8:47 am

Na; Alfred Bulahya.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. John Jingu ameitaka jamii, wadau kwa nafasi zao kupaza sauti dhidi ya vitendo vya ukatili ambavyo vimekuwa vikitokea  katika maeneo mbalimbali nchini.

Dkt. Jingu ameyasema hayo Jijini Dodoma kwa niaba ya Katibu Mkuu Kiongozi wakati akifungua kikao cha Makatibu Wakuu na Manaibu Makatibu  Wakuu kuhusu  mafunzo ya Usawa wa Kijinsia na Tathimini ya Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA).

Amesema pamoja na Juhudi mbalimbali ipo haja ya kuwa na afua mbalimbali za kuwatetea manusura wa vitendo hivyo.

.

Pia ameyabainisha masuala yaliyojadiliwa ni pamoja na kuwepo kwa Mpango maalumu wa malezi ya vijana balehe.

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake  na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula amewataka maafisa maendeleo kupitia ngazi ya Vijiji, Kata hadi Wilaya kutimiza wajibu wao.

.

Mratibu wa MTAKUWWA, Bw. Joel Mangi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake  na Makundi Maalum ameeleza kuwa kumekuwa pia na uanzishwaji wa vituo 21 vya huduma kwa manusura wa ukatili vinavyofanya kazi nchi nzima.

.