Wakulima Kondoa wanufaika na taarifa za hali ya hewa
2 March 2021, 1:41 pm
Na, Benard Filbert,
Dodoma.
Imeelezwa kuwa baada ya Halmashauri ya Mji wa Kondoa kuunganishwa katika mfumo wa taarifa wa mamlaka ya hali ya hewa nchini imesaidia wakulima kuendesha shughuli zao kuendana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Hayo yameelezwa na mkuu wa idara ya kilimo Kondoa mji Bw.Hassani Kiseto wakati akizungungumza na taswira ya habari kuhusu umuhimu wa taarifa za mamlaka ya hali ya hewa kwa wakulima.
Amesema kitendo cha kuunganishwa katika mfumo huo umesaidia wananchi kupata taarifa za mabadiliko ya hali ya hewa kila wiki hivyo kufanya kilimo kutokana na nyakati.
Mmoja wa wakulima kutoka Wilayani humo akizungumza na taswira ya habari amesema uwepo wa taarifa kila wiki kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa zimekuwa na msaada mkubwa ikiwepo kujua namna ya kukabiliana na shughuli mbalimbali za kilimo kuendana na mabadiliko hayo.