Imani potofu zina didimiza mapambano dhidi ya kifua kikuu
21 March 2022, 2:17 pm
Na; Yussuph Hassan .
Dhana ya kuhusisha ugonjwa wa kifua kikuu na imani potofu, imeelezwa kuwa dhana hiyo kwa kiasi kikubwa imekuwa ikididimiza juhudi za serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo.
Dhana hii ni kufatia baadhi ya jamii kuamini mgonjwa wa kifua kikuu kuwa amerogwa suala ambalo husabisha ugumu wa matibabu kwa wagonjwa hao.
Mratibu wa Kifua Kikuu Dodoma Peres Lukango anasema ugonjwa wa kifua kikuu ni ugonjwa unaosambazwa kwa njia ya hewa
Ameongeza kuwa sio lazima kila mwenye kifuu kikuu atakuwa na UKIMWI japokuwa magonjwa hayo mara nyingi yanaenda sambamba.
Taswira ya habari imezungumza na baadhi ya wakazi mkoani Dodoma ambapo kwa kiasi kikubwa wakazi wa mjini wanafahamu juu ya ugonjwa huo kwa kina.
Tanzania inazidi kupiga hatua katika kupunguza kasi ya maambukizi ya mapya ya ugonjwa wa kifua kikuu kwa asilimia 18% kwa mwaka 2020 kwa mujibu wa shirika la afya Duniani.