Mkoa wa Dodoma watajwa kuwa miongoni mwa mikoa ambayo bado imeshikilia mfumo Dume
28 September 2021, 1:29 pm
Na;Mindi Joseph .
Mkoa wa Dodoma umetajwa kuwa miongoni mwa mikoa ambayo wanawake hawashirikishwi katika maamuzi ya familia kutokana na uwepo wa mfumo dume.
Taswira ya habari imezungumza na Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Dodoma Bi.Honoratha Rwegasira amesema kuwa katika Mkoa wa Dodoma bado kuna changamoto ya wanawake hususani wa vijijini kutokupewa nafasi ya kushiriki katika maamuzi ya familia.
Ameongeza kuwa serikali inaendelea kufanya jitihada ya kutoa elimu kutatua changamoto hiyo kwani inarudisha nyuma maendeleo ya kaya.
Kwa upande wake Afisa jinsia kutoka shirika la Farm Africa Bi Helena Lawi anasema bado kuna changamoto katika ushirikishwaji wa maamuzi katika kilimo kwa wananwake licha ya Zaidi ya asilimia 72 kuwa ndio wanashiriki Zaidi katika kilimo.
Elimu inaendelea kutolewa na wadau mbalimbali kwa kushirikiana na ili kuimarisha maendeleo na kuondoa migogoro kwa familia inayojitokeza baada ya mazao kuvunwa.