Mwanamke ana haki ya kumiliki mali na kuuza chochote kwaajili ya familia
14 July 2021, 1:28 pm
Na; Shani Nicolous.
Imeelezwa kuwa mwanamke anahaki ya msingi ya kumiliki ardhi kama ilivyo kwa upande wa mwanaume katika familia kwa mjibu wa sheria.
Akizungumza na Dodoma fm msaidizi wa kisheria kutoka halmashauri ya Wilaya ya Bahi Bw. Yona Sakaza amesema kuwa wanawake wanahaki za kumiliki mali na kuuza chochote katika familia kwa ajili ya kuihudumia familia pamoja na haki zote anazostahili kisheria.
Amesema kuwa kwa miaka ya nyuma kulikuwa na baadhi ya makabila ambayo yalikuwa yakiamini dhana ya mwanamke kuto miliki mali na ilikuwa ni chanzo cha kutengeneza ubaguzi huo ingawa kwa sasa jamii imebadilisha mitazamo hiyo baada ya sheria mbalimbali za ndoa kuingilia kati dhana hiyo.
Kwa upande wake Mwajuma Mohammed pamoja na Bw. Nyemo Willson wamesema kuwa sheria ya ndoa inaelekeza sababu mbalimbali zinazopelekea ndoa kuvunjika hivyo ni vema wanandoa wakafahamu misingi na sheria hizo na kwamba baadhi ya kesi nyingi wanazozipokea nikutoka kwa wanandoa zinazosababishwa na wivu wa kimapenzi hali inayopelekea kusababisha kipigo hata kuvunja ndoa.
Msingi mizuri ya usawa katika jamii ndiyo sababu yakutengeneza mwendelezo mzuri wa haki baina ya jinsi ya kike na kiume hivyo ni vema elimu izidi kutolewa ili wananwake wapewe haki zao katika ndo ikifuatiwa na watoto wa jinsia zote mbili kupewa kipaumbele kwa baadhi ya maamzi katika familia na hata kurithishwa mali.