Wachimbaji wadogo wa madini watakiwa kutotumia zebaki
6 November 2024, 5:53 pm
Na Mariam Kasawa .
Wachimaji wadogo wa madini Nchini wameshauriwa kuachana na matumizi ya kemikali aina ya zebaki katika shughuli za uchenjuaji madini .
Kwa mujibu wa shirika la Afya Duniani WHO linasema kemikali ya zebaki kwamba ni miongoni mwa vyanzo kumi hatarishi kwa afya za binadamu na mazingira pia.
Bwn. Christopher Kadeo mchimbaji mdogo wa madini ya dhahabu kutoka Geita amesema kuwa mafunzo yanapaswa kuendelea kutolewa kwa wachimbaji wadogo ili wafahamu madhara na hasara ya kutumia kemikali ya zebaki katika uchenjuaji wa madini.
Mkutano wa nchi za Afrika zinazotekeleza Mradi wa Kudhibiti Matumizi ya Zebaki kwa Wachimbaji Wadogo wa Dhahabu (EHPMP), unafanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Novemba 4 hadi nov 12, 2024.
Mradi huu unatekelezwa katika Nchi tano barani Afrika ambazo ni Tanzania, Kenya, Senegal, Zambia na Ghana, pia unahusisha masuala ya usimamizi wa taka za kielektroniki kwa baadhi ya nchi.