Wachimbaji wadogo wa madini kuachana na matumizi zebaki
5 November 2024, 5:57 pm
Na Mariam Kasawa.
Wachimbaji wadogo wa madini nchini wametakiwa kuachana na matumizi ya kemikali ya zebaki (Mercury) na kutumia teknolojia mbadala kwenye uchenjuaji wa dhahabu ili kulinda afya ya binadamu na Mazingira.
Dkt. Immaculate Sware Semesi Mkurugenzi Mkuu NEMC akiwa katika mkutano wa kikanda wa nchi za Afrika zinazotekeleza Mradi wa Kudhibiti Matumizi ya Zebaki kwa wachimbaji wadogo wa dhahabu (EHPMP) anaelezea athari zinazotokana na zebaki pamoja na jinsi walivyojipanga kuachana na matumizi ya kemikali hiyo. .
Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhandisi. Cyprian Luhemeja alifungua Mkutano wa Kikanda wa Nchi za Afrika zinazotekeleza Mradi wa Kudhibiti Matumizi ya Zebaki kwa wachimbaji wadogo wa dhahabu (EHPMP) Nov. 4, 2024 anaeleza zaidi malengo ya mkutano huo.
.