Dodoma FM

Shule ya Msingi Idilo yafaidika na mapato ya Kijiji

23 October 2024, 12:55 am

Na Noel Steven.

Shule ya msingi  Idilo imeafaidika  na kwa kupata msaada wa madawati 30 kutokana  na miradi  ya uwekezaji katika kijiji hicho.

Zaidi ya Wanafunzi 90 waliokuwa wakisoma huku wamekaa chini Katika shule ya Msingi Idilo wameondokana na adha hiyo baada ya serikali ya Kijiji kutengeneza madawati  30.

Mkuu wa shule hiyo Bwn. Majuto Mlowosa amasema walikuwa wanakabiliwa na upungufu mkubwa wa madawati ambapo wanafunzi walilazimika  kusoma huku wamekaa chini.  

Mkuu wa shule hiyo Bwn. Majuto Mlowosa
Sauti ya Bwn. Majuto Mlowosa

Kwa upande wa wanafunzi wanaeleza jinsi madawati hayo yatakavyosaidia kuwaweka safi wakati wa masomo

Sauti za wanafunzi

Aidha Mtendaji wa kijiji hicho Bi. Victoria Lesilwa amesema madawati hayo yametengenezwa na fedha kutoka kwenye vyanzo vya mapato ya kijiji .

Mtendaji wa kijiji hicho Bi. Victoria Lesilwa
Sauti ya Bi. Victoria Lesilwa
Pichani moja ya mzazo wa kijiji cha Idilo
Sauti ya mwanachi