Dodoma FM

Madini yapata vitendea kazi kudhibiti upotevu

21 October 2024, 7:35 pm

Na Mariam Kasawa.

Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amezindua magari mapya 25  yalilyotolewa na serikali kama vitendea kazi ili kutimiza lengo la makusanyo ya mapato na udhibiti wa utoroshaji wa madini.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo, octoba 21 Mhe. Mavunde amesema kuwa magari hayo ni kwa ajili ya mpango wa uboreshaji wa usimamizi wa Sekta ya Madini.

Pichani waziri wa madini Mhe. Anthony Mavunde akizindua magari 25
Sauti ya Mhe. Anthony Mavunde

Aidha Mhe. Mavunde ameelekeza magari hayo  yafungwe GPS kwa ajili ya kuangalia mwenendo wake ili kuhakikisha yanatumika katika matumizi yaliyokusudiwa.

Pichani ni aina ya magari Toyota Landcruiser yaliyozinduliwa na Mhe. Mavunde