Dodoma FM

TANZIA: PCMA wamlilia Askofu Mondeya

18 October 2024, 8:04 pm

Na Nazael Mkude.

Wachungaji na waamini wa kanisa la PCMA Mkoani Dodoma  wamepokea kwa masikitiko kifo cha Askofu Mkuu  Dr.  Mondea Kabeho

Katibu Mkuu wa Kanisa la hilo Patrick Kajila anaelezea jinsi msiba huo ulivyotokea wakati wa ibada ya kuwafariji wafiwa iliyofanyika katika kanisa hilo Mtaa wa Nzuguni A.

Pichani Katibu Mkuu wa Kanisa la PCMA Patrick Kajila akieleza jinsi msiba ulivyotokea
Sauti ya Bwn. Patrick Kajila

Aidha waombolezaji wamemuelezea marehemu kuwa alikuwa ni mtu wa watu na mpenda haki na atakumbukwa daima kwa mazuri yake.

Pichani waombolezaji wakiwa wamekusanyika nyumbani kwa marehemu
Sauti ya waombolezaji

Mazishi ya mwili wa aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la PCMA Tanzania yatafanyika siku ya Oct. 18 2024 jijini Dar es Salaam majira ya mchana.