Dodoma FM

Watu wenye ulemavu ni chachu ya maendeleo jumuishi

17 October 2024, 8:01 pm

Na Mariam Matundu.

Katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa nov. 27 kundi la watu wenye ulemavu limetajwa kuwa ni kundi muhimu kushiriki katika mchakato huu kwa kupiga kura na kugombea nafasi zilizopo ili kuchochea maendeleo yenye ujumuishi.

Afisa maendeleo Halmashauri ya wilaya ya Chamwino B.i Zaina Msangi amesema hayo wakati akielezea umuhimu wa kundi hilo kutokuachwa nyuma .

Afisa Maendeleo Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino B.i Zaina Msangi
Sauti B.i Zaina Msangi

kwa upande wake Mwenyekiti wa Shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu wilaya ya Chamwino Bwn. John Tongoo Peter amesema ili kuwepo ushiriki wa kudi hilo la wenye ulemavu ni lazima kuwepo na uhamasishaji unaoendana na mahitaji ya makundi yote ya wenye ulemavu.

Mwenyekiti wa Shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu Wilaya ya Chamwino Bwn. John Tongoo Peter
Sauti ya Bwn. John Tongoo

Kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) watu wenye ulemavu ni takribani asiimia 9.3 ya watu wote hapa nchini ambapo ni sawa na watu milioni 3.3. na kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi ya mwaka 2019 zaidi ya watu 300 walishinda nafasi mbalimbali za uongozi .