Dodoma FM

Wananchi wataharuki tukio la mtu kujinyonga Dodoma

17 October 2024, 8:01 pm

Na Nazael Mkude.

Wakazi wa Mtaa wa Mathias Kata ya Miyuji Mkoani Dodoma wamepatwa na taharuki baada  ya tukio la mtu mmoja kujingonga katika mtaa huo .

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Balaozi Shina Namba 5 wa Mtaa wa Mathias Bwn.  Said Ali Madeni anasema kuwa  marehemu alikuwa ni jirani yake ambaye alikuwa ni fundi ujenzi.

Balaozi Shina Namba 5 wa Mtaa wa Mathias Bwn.  Said Ali Madeni
Sauti ya Bwn. Mathias Said Ali Madeni

Bwn. Sulemani Zebedayo Mazego  Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Mathias Kata ya Miyuji anaelezea jinsi alivyopata taarifa na hatua walizozichukua.

Bwn. Sulemani Zebedayo Mazego  Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Mathias Kata ya Miyuji
Sauti ya Bwn. Sulemani Zebedayo Mazego  

Wakiwa katika hali ya taharuki, baadhi ya wakazi wa mtaa huo ambao wanamfahamu marehem wamesilitishwa kutokea kwa tukio hilo.

Pichani mwananchi akieleza masikitiko yake juu ya tukio la kujinyonga
Sauti za wananchi
Pichani moja ya jirani wa marehemu akieleza jinsi anavyomfahamu marehemu

Wakati huo Jeshi la Polisi limechukua nafasi hiyo kuwaasa wananchi kuwa wazi kwa wenza wao endapo watakuwa wanakabiliwa na changamoto binafsi zinazopelekea msongo wa mawazo . Tukio hilo limetokea oktoba 16, 2024 ambapo marehemu alifahamika kwa jina la Stanslaus Samira Osebio mwenyeji wa Iringa.

Pichani Polisi Kata akitoa nasaha mbele ya waombolezaji juu ya tukio la kujinyonga
Sauti ya Polisi Kata