Dodoma FM

Hakuna tozo kuandikisha au kuboresha taarifa daftari la mpiga kura

27 September 2024, 8:42 pm

Na Mindi Joseph.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Rosemary Senyamule ameonya juu ya upotoshaji unaofanywa na baadhi ya watu kuhusu mwenendo wa zoezi la uandikishaji wananchi katika daftari la kudumu la mpiga kura .

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mh. Senyamule amesema hakuna malipo yoyote ambayo mwananchi anatakiwa kutozwa ili aweze kuandikishwa au kuboresha taarifa zake katika daftari la kudumu la mpiga kura.

Sauti ya Mh. Rosemary Senyamule

Mh. Senyamule amewataka wananchi kutofautisha mchakato wa uandikishaji wa daftari la kudumu la mpiga kura na mchakato wa maandalizi ya kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa ambao unatarajiwa kufanyika mwezi novemba mwaka huu.

Sauti ya Mh. Rosemary Senyamule

Zoezi la ujiandikishaji na uboreshaji wa taarifa za mpiga kura katika wilaya nne za Mkoa wa Dodoma limeanza 25 Septemba 2024 na litafikia ukomo October mosi mwaka huu ambapo wapiga kura wapya 845,976 wanatarajiwa kuandikishwa na idadi ya jumla ya wapiga kura ikikadiriwa kufikia 1777,834