Dodoma FM

Utaratibu wa daftari la makazi kinga dhidi ya mauaji Dodoma

20 September 2024, 7:50 pm

Na Nazael Mkude

Wakazi jijini Dodoma wametoa maoni yao kuhusu utaratibu wa kujiandikisha katika daftari la makazi ili kuweza kupunguza vitendo vya uvunjifu wa sheria.

Kufuatia mwendelezo wa matukio ya kihalifu ya mara kwa mara yanayotokea katika jiji la Dodoma,  wananchi wameiomba serikali kurudisha utaratibu wa kujiorodhesha katika daftari maalum la makazi.

Bi Mariam Mlewa
Sauti ya Bi Mariam Mlewa
Bwn Hamisi
Sauti ya Bwn, Hamisi

Bwn. Abel Majiko
Sauti ya Bwn. Abel Majiko

Aidha wenyeviti wa mitaa pamoja na mabalozi wamesema kuwa ili kupunguza mauji na matukio yanayotokea kwa baadhi ya maeneo ya jiji la Dodoma utaratibu wa daftari la makazi utasaidia kuwatambua wakazi husika pamoja na wageni wanaohamia au kuishi kwa muda katika maeneo ya makazi.

Mohammed Ramadhani Misanga M/kiti Mtaa wa Chidachi Kata ya Mkonze

Maoni ya kurejeshwa  kwa  utaratibu wa daftari la kudumu la mkazi  yanatokana na kujitokeza kwa  matukio ya mauaji na uhalifu ya mara kwa mara  katika  jiji la Dodoma.

Sauti ya Mohammed Ramadhani Misanga