Dodoma FM
Dhana ya Kubemenda ni Batili
9 September 2024, 7:51 pm
Na Yusufu Hassan. Dhana ya kubemendwa kwa mtoto ambayo inayohusishwa na kuathiri makuzi ya mtoto, ambapo jamii huamini kuwa mtoto aliyebemendwa hupata kubemendwa changamoto kadhaa katika ukuaji wake.
Jamii imefika mbali zaidi hata kuwakejeli watoto wanaodhaniwa kuwa wamebemendwa na kwa kuwaita mafundi viatu kutoka na muonekano wao unaosababishwa na changamoto za ukuaji.
Daktari Matthew Gaudance kutoka Decca Polyclinic anatolea ufafanuzi juu ya dhana hii ya kubemendwa kwa kuelezea ni nini jamiii huamini katika dhana hii pamoja na usahihi wake.