NaCoNGO watakiwa kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia sheria
26 June 2024, 5:50 pm
Sekta Binafsi nchini zimekuwa na mchango katika kuchangia ukuuaji wa uchumi wa Taifa.
Na Mindi Joseph.
Baraza la Taifa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali NaCoNGO limetakiwa kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia sheria ili kukidhi matarajio ya Jamii na Taifa.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia wanawake na Makundi Maalum Dkt Dorothy Gwajima ameyasema hayo Leo katika uzinduzi wa baraza hilo.
Mashirika haya yanamchango gani katika maendeleo ya Jamii hapa wadau wanasema.
Mashirika yasiyo ya kiserikali hufanya kazi katika nyanja mbalimbali ikiwemo Afya,Elimu,Kilimo na sekta nyingine Msajili wa Mashirika hayo Vickness anabainsha.
Mwenyekiti Wa Baraza La Mashirika Yasiyokuwa Ya Kiserikali NaCoNGO Gasper Makala atahakikisha mashirika yanafanya kazi kwa kuzingatia sheria.