Wananchi watakiwa kufahamu sheria za utatuzi wa migogoro
23 January 2024, 7:32 pm
Maonesho ya wiki ya sheria yanatarajia kuanza kesho januari 24 jijini dodoma na ufunguzi huo utafanywa na Spika wa bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Akson huku kilele chake kikiwa januari 31 na mgeni Rasmi akitarajiwa kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani.
Na Fred Cheti.
Wito umetolewa kwa wananchi kujifunza na kufahamu sheria mbalimbali ili ziwawezeshe kupata suluhu ya migogoro badala ya kusubiri kutokea kwa mgogoro ndipo waanze kutafuta misaada ya kisheria.
Rai hiyo hiyo imetolewa na Bw. Charles Magesa Naibu msajili wa mahakama ya rufani ambae pia ni katibu wa kamati ya maandalizi ya maonesho ya wiki ya sheria kwa mwaka 2024 wakati akizungumza katika kipindi cha The Morning Power Show kuelekea ufunguzi wa maonesho hayo yanayotarajia kuanza kesho katika viwanja vya Nyerere Square jijini hapa.
Aidha amesema katika maonesho hayo wananchi watapata huduma mbalimbali za kisheria ikiwemo elimu itakayotolewa kupitia taasisi mbalimbali zinazohusika na utoaji wa huduma za msaada wa kisheria.
Dodoma tv imezungumza na baadhi ya wananchi jijini dodoma na kuwahoji juu ya mwamko wa jamii kutaka kufahamu sheria mbalimbali.