Waganga wa wilaya watakiwa kutumia vema magari ya yaliyo tolewa na serikali
20 December 2023, 1:46 pm
Ikumbukwe Dodoma ina jumla ya Vituo vya afya 545 ambapo hospitali ni 16,Vituo vya afya 63,zahanati 438 na kliniki maalum 26 .
Na Mariam Kasawa.
Waganga wakuu wa wilaya wametakiwa kutumia Vyema magari yaliyotolewa na Serikali kwa ajili ya kwenda kusimamia na kuhakikisha huduma bora zinatolewa kwa wananchi kuanzia ngazi ya kijiji.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Mohamed Mchengerwa wakati akikabidhi magari matano kwa ajili ya shughuli za Usimamizi wa Huduma za afya kwa Mkoa wa Dodoma ambapo amesisitiza Waganga wakuu wa wilaya kutumia magari hayo kwenda kusikiliza kero za watumishi katika sekta ya afya.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amesema kupatikana kwa magari hayo yatasaidia kuimarisha shughuli za usimamizi wa miradi ya afya na kusaidia utoaji wa huduma za afya ,ustawi wa jamii na lishe katika ngazi ya halmashauri na vituo vya kutolea huduma za afya.
Mkoa wa Dodoma una mahitaji ya magari 79 ya kubeba wagonjwa ambapo hadi kufika disemba 2023 mkoa ulikuwa na jumla ya magari 27 sawa na asilimia 34 .