Magonjwa yasiyoambukiza huchangia asilimia 33 ya vifo nchini-WHO
18 December 2023, 9:43 pm
Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo wananchi huathirika zaidi na magonjwa yasiyoambukiza.
Na Fred Cheti.
Kwa mujibu wa takwimu kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaeleza kuwa magonjwa yasiyoambukiza yanachangia takribani asilimia 33 ya vifo vyote nchini huku takwimu hizo zikionesha kuwa kwa mwaka 2020 pekee magonjwa hayo yalichangia zaidi ya vifo milioni 41 sawa na asilimia 71 duniani kote.
Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo wananchi huathirika zaidi na magonjwa yasiyoambukiza huku moja ya sababu inayotajwa kuchangia magonjwa hayo ni pamoja na mfumo wa maisha ya binadamu.
Katika kuendelea kutoa elimu juu ya kujikinga na magonjwa Bw. Paul Njige mwanafunzi wa kozi ya famasia kutoka chuo cha St. John kilichopo jijini Dodoma ambaye pia ni makamu wa rais wa umoja wa wanafunzi wa kozi ya famasia nchini (TAPSA) anaeleza hatua za kuchukua ili kujikinga na magonjwa hayo wakati akizungumza katika kipindi cha The Morning Power Show.
Kwa upande wake Doberah Luvanda anaeleza sababu ambazo huchangia mtu kupata magonjwa hayo na jinsi gani anaweza kuepuka kuyapata.