Watekelezaji wa mpango wa makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto watakiwa kutenga bajeti
12 December 2023, 9:04 am
Mkutano huo umezinduliwa leo jijini Dodoma ambapo umeambatana na ufungunguzi wa Mwongozo Jumuishi wa Taifa wa Utekelezaji wa Mpango wa (PJT-MMMAM).
Na Mwandishi wetu.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Dkt. Dorothy Gwajima ametoa rai kwa watekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Malezi Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (MMMAM) kuhakikisha wanatenga bajeti ili kufanikisha malengo ya mpango huo.
Ametoa Rai hiyo wakati akifungua Mkutano wa Kitaifa wa Wadau wa mpango wa sekta zote sambamba na kuzindua Mwongozo Jumuishi wa Taifa wa Utekelezaji wa Mpango huo (PJT-MMMAM) Jijini Dodoma.
Waziri Dkt. Gwajima amesema Wizara inatambua umuhimu wa Wadau katika utekelezaji wa PJT MMMAM ambapo amewataka kuainisha vipaumbele kwa uratibu wa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa ili kuingizwa kwenye bajeti ya Serikali ya 2024/25.
Amewataka kufanya kazi kama timu kwa kuwa malengo ya programu ya MMMAM hayawezi kufikiwa bila kuzishirikisha sekta zote kwa uwiano na umuhimu unaofanana.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Children in Crossfire Bw.Craig Ferla amesema mpaka sasa hivi mikoa yote 26 nchini imezindua programu ya MMMAM, na pia takribani halmashauri 70 na malengo yako kwa mwakani mwezi Machi,2024 kuweza kufikia halmashauri zote Tanzania.