Watu wenye ulemavu watakiwa kuripoti vitendo vya ubaguzi ili haki itendeke
4 December 2023, 3:57 pm
Maadhimisho ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu huadhimishwa kila ifikapo Desemba 3 ambapo kaulimbiu ya mwaka huu ni “Tuungane kuchukua hatua katika kutoa huduma ili kuyafikia malengo ya maendeleo endelevu kwa watu wenye ulemavu”
Na Victor Chigwada.
Watu wenye ulemavu wametakiwa kuacha kukaa kimya pale wanapoona haki haitendeki ili kuleta usawa .
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu), Patrobas Katambi alipohudhuria kongamano la watu wenye ulemavu lililofanyika katika Kata ya Mtumba jijini Dodoma.
Katambi amesema ni vema watu wenye ulemavu kutoa ushirikiano kwa wizara husika ila kuleta suluhu ya mambo yanayojiri na ambayo yalishajadiliwa ili kupatiwa ufumbuzi.
Pia amesema kuwa hakuna vikwazo wala sababu zozote zinazoweza kukwamisha utekelezaji wa sera kwa watu wenye ulemavu
Katambi ameongeza kuwa changamoto ya mmomonyoko wa maadili imekuwa ikichangia kwa kiasi kubwa ukatili kwa watu wenye ulemavu.