Jiji la Dodoma latakiwa kuangalia vyanzo vipya vya mapato
1 November 2023, 12:08 pm
Katika Mwaka wa fedha 2023/24 Halmashauri ya Jiji la Dodoma imekisia kukusanya na kutumia jumla ya shillingi 132,401,769,120 ambapo robo ya kwanza ya mwaka 2023 kuanza julai- septemba mapato yaliokusanywa ni 30,879,168,799.
Na Yussuph Hassan.
Halmshauri ya Jiji la Dodoma imetakiwa kuangalia vyanzo vipya vya mapato katika kuhakikisha Dodoma inafikia malengo ya ukusanyaji wa mapato.
Hili linamkutanisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule na viongozi mbalimbali ndani ya Jiji la Dodoma kujadili namna ya kufikia mapato hayo.
Kupitia taarifa ya utekelezaji na utendaji kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2023/24 Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri amepongeza changamoto mbalimbali zilizoshughulikiwa.
Kwa upande wao viongozi na wakuu wa idara kutoka halmashauri ya jiji la Dodoma wameahidi kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza kasi ya ukuwaji wa jiji la Dodoma.
Halmashauri ya jiji la Dodoma imekisia kukusanya na kutumia bilioni 132,401,769,120 huku ripoti ya utekelezaji na utendaji kazi kwa kipindi cha kuanzia Julai-Septemba 2023 ni bilioni 30,879,168,799 kupitia mapato ya ndani ya jiji, ruzuku ya mishahara, ruzuku ya matumizi mengineyo na ruzuku ya miradi ya maendeleo.